عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمِنينَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا:
كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَجْتَهِدُ فِي الْعَشْرِ الْأَوَاخِرِ مَا لَا يَجْتَهِدُ فِي غَيْرِهِ.
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1175]
المزيــد ...
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1175]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake zinapokuja siku kumi za mwisho wa ramadhani anajitahidi ndani yake kwa kufanya ibada na utiifu, na akipitiliza katika kufanya aina mbalimbali za kheri na aina za wema na ibada zaidi kuliko namna anavyojitahidi katika siku zingine; na hii ni kwa sababu ya utukufu na fadhila za siku hizi, na ni kwa sababu ya kuitafuta Lailatul Qadri (usiku wa cheo).