عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «كل أُمتي مُعَافًى إلا المُجاهرين، وإنَّ من المُجَاهرة أن يعملَ الرجلُ بالليل عملًا، ثم يُصْبِح وقد سَتره الله عليه، فيقول: يا فلان، عَمِلت البَارحة كذا وكذا، وقد بَات يَسْتُره ربه، ويُصبح يَكشف سِتْرَ الله عنه».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Umma wangu wote watasalimika isipokuwa wenye kuyatangaza (madhambi), Na hakika katika sehemu ya kuyatangaza ni mtu kufanya jambo usiku, kisha akaamka hali yakuwa Mwenyezi Mungu kamsitiri, akasema: Ewe fulani nilifanya jana usiku kadhaa wa kadhaa, haliyakuwa alilala akiwa kasitiriwa na Mola wake, na anaamka anafunua sitara ya Mola wake kwake".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Waislamu wote amewasamehe Mwenyezi Mungu isipokuwa atakayeifedhehesha nafsi yake, kwa kufanya maasi usiku akamsitiri Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha anaamka anawaeleza watu, Mwenyezi Mungu anamsitiri kisha yeye anaifedhehesha nafsi yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama