عن أبي بكرة نفيع بن الحارث الثقفي رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «إذا التَقَى المسلمانِ بسَيْفَيْهِمَا فالقاتلُ والمقْتُولُ في النَّارِ». قلت: يا رسول الله، هذا القاتلُ فما بالُ المقتولِ؟ قال: «إنه كان حريصًا على قَتْلِ صَاحِبِهِ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abii Bakra Nufa'i bin Harith Ath thaqafiy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake Amesema: "Watakapo kutana waislamu wawili kwa mapanga yao basi muuwaji na muuliwaji wote motoni" Nikasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, huyu muuwaji sawa, na vipi huyu muuliwaji? Akasema: "Hata yeye alikuwa na pupa ya kumuuwa mwenzie".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Watakapo kutana waislamu wawili kwa mapanga yao, akiwa kakusudia kila mmoja wao kummaliza mwenzie; muuwaji motoni kwasababu ya kuhusika kumuuwa mwenzie, na muuliwaji pia motoni kwasababu ya pupa yake na yeye juu ya hilo, ikiwa Mwenyezi Mungu hatowasamehe, na kunapokuwa kupigana si kwa haki, kama ilivyokuja katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ikiwa litakengeuka kundi moja kati ya mawili, basi lipigeni lililokengeuka mpaka lirudi katika amri ya Mwenyezi Mungu".

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kupatikana adhabu kwa yeyote atakayedhamiria kufanya maasi kwa moyo wake na akaithibitisha nafsi yake juu yake na akafanya sababu zake; sawa sawa yametokea au hayajatokea, ikiwa Mwenyezi Mungu hatomsamehe, ama atakayepania moyoni mwake tu na akawa hajafanya sababu hapati dhambi.
  2. Tahadhari ya kupigana waislamu.