عن أبي بَكْرَةَ- رضي الله عنه - عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: «أَلا أُنَبِّئُكم بِأَكْبَرِ الْكَبَائِر؟»- ثَلاثا- قُلْنَا: بَلى يا رسول الله، قَالَ: «الإِشْرَاكُ بِالله وَعُقُوقُ الوالدين، وكان مُتَّكِئاً فَجَلس، وَقَال: ألا وَقَوْلُ الزور، وَشهَادَةُ الزُّور»، فَما زال يُكَرِّرُها حتى قُلنَا: لَيْتَه سَكَت.
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abii Bakrata- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume- rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye amesema: "Je nisikuelezeni juu ya madhambi makubwa kuliko yote?" -Akarudia hivyo mara tatu- tukasema: Ndiyo, tueleze Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na alikuwa kaegamia akakaa, na akasema: tahadharini! na kusema uongo, na kutoa ushuhuda wa uongo" Hakuacha kulirudia hilo mpaka tukasema: Laiti angenyamaza.
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Yakwamba Mtume rehema na Amani zimfikie alisema kuwaambia maswahaba zake, Je nisikuelezeni? yaani nikuelezeni madhambi makubwa kuliko yote, akataja haya matatu ambayo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, nako nikufanya uadui katika cheo cha uungu,na ni kuchukua haki yake Allah alie takasika na kutukuka, na kumpa asiestahiki katika viumbe wenyekushindwa (wasio na uwezo), na kuwaasi wazazi ni dhambi mbaya mno, kwasababu ni kulipa wema kwa ubaya tena kwa mtu wa karibu, na kushuhudia uongo kunajumuisha kila kauli ya kutengenezwa na ya uongo, inayokusudiwa kumdhalilisha yule iliyeangukia kwake, kwa kuchukua mali yake, au kuvunja heshima yake, na mfano wa hayo.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani Pashto
Kuonyesha Tarjama

من فوائد الحديث

  1. Inachukuliwa faida katika hadithi hii, kufikisha hukumu za sheria kwa njia ya kutanabahisha kama alivyo sema Mtume: "Je nisikuelezeni"
  2. Hakika dhambi kubwa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kwasababu yeye ameifanya(shirki) kuwa ndiyo chimbuko la madhambi makubwa na kubwa lao, na inalitilia mkazo hili kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa, na anasemehe madhambi yasiyokuwa shirki kwa amtakaye"
  3. Ukubwa wa haki ya wazazi wawili,ni pale alipoiambatanisha haki yao na haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Hatari ya kushuhudia uongo, na athari yake mbaya katika jamii ya kiislamu; sawasawa iwe upande wa kitabia au upande mwingine, katika muonekano wa maisha ya kijamii.