عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِذَا جَمَعَ اللهُ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرْفَعُ لِكُلِّ غَادِرٍ لِوَاءٌ، فَقِيلَ: هَذِهِ غَدْرَةُ فُلَانِ بْنِ فُلَانٍ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1735]
المزيــد ...
Kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake:
"Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1735]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama atakapowakusanya wa mwanzo na wa mwisho kwa ajili ya hesabu, atasimika kwa kila haini ambaye hakutimiza ahadi aliyokubaliana nayo kwa Mwenyezi Mungu au pamoja na watu, alama ambayo atamfedhehesha kwayo mbele za watu kwa sababu ya hiana yake, na kutanadiwa juu yake siku hiyo: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani; kwa ajili ya kutangaza ubaya wa kitendo chake mbele ya waliokusanyika katika uwanja halaiki (mahashari).