عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعا: "قال تعالى : أنا أغنى الشركاء عن الشرك؛ من عمل عملا أشرك معي فيه غيري تركتُه وشِرْكَه".
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Hadithi Marfu'u: "Amesema -Mtukufu- Mimi nimejitosheleza na washirika juu ya kushirikishwa; atakayefanya jambo lolote akamshirikisha pamoja nami mwingine nitamuacha na shirki yake au (na mshirika wake)."
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim
Anapokea rehema na Amani zimfikie kutoka kwa Mola wake Mtukufu- Na huitwa hadithil Qudsiy- Kuwa yeye anajiepusha na amali yoyote ambayo imeingiwa ushirika na yeyote kwa kujionyesha au kwa kingine; kwasababu yeye Mtukufu hakubali ispokuwa yale yaliyotakasiwa nia kwa kutaka radhi zake.