عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قال:
قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم كَلِمَةً وَقُلْتُ أُخْرَى، قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: «مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَدْعُو مِنْ دُونِ اللهِ نِدًّا دَخَلَ النَّارَ» وَقُلْتُ أَنَا: مَنْ مَاتَ وَهُوَ لَا يَدْعُو لِلهِ نِدًّا دَخَلَ الْجَنَّةَ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4497]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Alisema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- neno moja nami nikasema neno jingine, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekufa hali yakuwa anaomba kinyume na Mwenyezi Mungu mungu mwingine, ataingia motoni" Na mimi nikasema: Atakayekufa hali yakuwa haombi mungu mwingine ataingia peponi.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4497]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeelekeza chochote katika vile ambavyo vinapasa kuwa vya Mwenyezi Mungu pekee kwa asiyekuwa yeye, kama kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kutaka msaada kwa asiyekuwa yeye, na akafa katika hali hiyo basi huyu ni katika watu wa motoni. Na akaongeza bin Masuod radhi za Allah ziwe juu yake kuwa atakayekufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote basi mafikio yake ni katika pepo.