عن عبد الله بن مسعود قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«هَلَكَ الْمُتَنَطِّعُون» قالها ثلاثًا.

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2670]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah Ibn Masoud amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Wameangamia wenye kufanya uzito katika mambo" Alisema hivyo mara tatu.

[Sahihi] - [Imepokelewa Imamu Muslim] - [Swahiih Muslim - 2670]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kufeli na kupata hasara kwa watiao ugumu -pasina uongofu wala kuwa na elimu- katika dini yao na dunia yao, na katika kauli zao na matendo yao, wenye kuvuka mipaka ya sheria aliyokuja nayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa misimamo mikali katika mambo yote, na himizo la kuepuka hilo katika kila kitu; hasa hasa katika ibada na kuwatukuza watu wema.
  2. Kutafuta ukamilifu katika ibada na mengine mazuri; na kunakuwa kwa kufuata sheria.
  3. Inapendeza kulitilia mkazo jambo muhimu, kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikariri sentensi hii mara tatu.
  4. Upole wa uislamu na wepesi wake.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (67)
Ziada