عن ابن عباس رضي الله عنهما في قول الله تعالى : (وَقَالُوا لا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلا سُوَاعًا وَلا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا) قال: "هذه أسماء رجال صالحين من قوم نوح، فلما هَلَكوا أَوحى الشَّيطان إلى قَومِهِم أنِ انْصِبُوا إلى مَجَالِسِهِم الَّتي كانوا يَجْلِسون فيها أنصَابًا، وسَمُّوها بأسمَائِهِم، فَفَعَلُوا، ولم تُعْبَد، حتَّى إِذَا هَلَك أُولئك ونُسِيَ العلم عُبِدت".
[صحيح] - [رواه البخاري]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ibn Abbas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao-Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema msiwaache waungu wenu, wala msimuache Wadd, wala Suwa'u wala Yaghuth na Yauq na Nasr" Akasema: "Haya ni majina ya watu wema katika watu wa Nuhu, walipokufa shetani aliwajulisha watu wao kuwa wekeni katika vikao vyao ambavyo walikuwa wakikaa hapo masanamu, na yaiteni kwa majina yao, wakafanya hivyo, na hayakuabudiwa, mpaka walipokufa hao na elimu ikasahaulika yakaabudiwa".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
Ana tafsiri Ibn Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Aya hii tukufu kuwa miungu hii ambayo ameitaja Mwenyezi Mungu Mtukufu- Kuwa watu wa Nuhu waliusiana kuendelea kuiabudu baada ya kuwa amewakataza Nabii wao Nuhu ziwe juu yake sala na salamu- kutomshirikisha Mwenyezi Mungu- kuwa majina hayo asili yake ni majina ya watu wema miongoni mwao, walichupa mipaka ndani yake kwa ushawishi wa Ibilisi kwao mpaka wakatundika picha zao, Basi jambo likakuwa katika picha hizi mpaka yakawa masanamu yanaabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu.