عن عطاء بن يسار وأبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: "اللهم لا تجعل قبري وثنا يُعبد، اشتد غضب الله على قوم اتخذوا قبور أنبيائهم مساجد".
[صحيحان] - [حديث عطاء بن يسار: رواه مالك.
حديث أبي هريرة رضي الله عنه: رواه أحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa A'twaa bin Yasari na Abuu Huraira- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Ewe Mola wangu usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu lenye kuabudiwa, zimekuwa kali hasira za Mwenyezi Mungu juu ya watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti.
Sahihi - Imepokelewa na Ahmad
Aliogopea rehema na Amani ziwe juu yake kutokea katika umma wake pamoja na kaburi lake yaliyojitokeza kwa Mayahudi na Wakristo pamoja na makaburi ya Manabii wao katika kuchupa mipaka juu yake, mpaka yakawa ni masanamu yenye kuabudiwa, Akamuomba Mola wake asilifanye kaburi lake hivyo, kisha akatahadharisha rehema na Amani zimfikie juu ya sababu iliyopelekea kupata ghadhabu kali na laana kwa Mayahudi na Wakristo, yale waliyoyafanya katika haki za makaburi ya Manabii wao mpaka wakayageuza kuwa masanamu yenye kuabudiwa, wakaingia katika shirki kubwa yenye kwenda kinyume na tauhidi.