عن جابر رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم سئل عن النُّشْرَةِ؟ فقال: هي من عمل الشيطان.
[صحيح] - [رواه أبو داود وأحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Jaabir radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-Yakwamba Mtume rehema na Amani zimfikie aliulizwa kuhusu Nushra (kutibu uchawi kwa uchawi)? Akasema: Hiyo ni katika kazi za shetani.
Sahihi - Imepokelewa na Abuu Daud

Ufafanuzi

Nikuwa Mtume rehema na Amani ziwe juu yake - Aliulizwa kuhusu kumtibu aliyerogwa kwa njia ambayo walikuwa wakiijua tangu zama za ujinga, mfano: kuondoa uchawi kwa uchawi ni ipi hukumu ya hilo, akajibu rehema na Amani zimfikie kuwa hiyo ni katika kazi za shetani, au hufanyika kupitia yeye; kwasababu inakuwa kwa aina ya uchawi na kwa kuwatumia mashetani, hiyo ni ushirikina na ni haramu. na ama kutibu uchawi kunakofaa: ni kuufungua uchawi kwa kisomo cha ruqya au kuutafuta, na kuufungua kwa mkono pamoja na kusoma Qur'ani au kwa dawa za halali.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani
Kuonyesha Tarjama

Faida nyingi

  1. Sheria ya kuwauliza wanachuoni katika yale yanayotatiza hukumu yake; kwa tahadhari ya kutoangukia katika haramu.
  2. Katazo la kutibu uchawi kwa namna wanayoifahamu watu wa zama za ujinga; kwasababu ni uchawi na uchawi ni ukafiri.
  3. Nikuwa kazi za shetani zote zimeharamishwa.