عن جندب بن عبد الله رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم قبل أن يموت بخمس، وهو يقول: «إني أبرأ إلى الله أن يكون لي منكم خليل، فإن الله قد اتخذني خليلا كما اتخذ إبراهيم خليلا، ولو كنت متخذا من أمتي خليلا لاتخذت أبا بكر خليلا، ألا وإن من كان قبلكم كانوا يتخذون قبور أنبيائهم مساجد، ألا فلا تتخذوا القبور مساجد، فإني أنهاكم عن ذلك».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Jundub bin Abdillah radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Amesema: Nilimsikia Mtume rehema na Amani zimfikie kabla hajafa kwa siku tano: naye akisema: "Hakika mimi najiepusha kwa Mwenyezi Mungu kuwa kwangu kati yenu na rafiki wa ndani, kwani Mwenyezi Mungu amenifanya mimi kuwa kipenzi wa ndani kama alivyomfanya Ibrahim kuwa kipenzi wa ndani, na lau kama ningejifanyia kipenzi wa ndani katika umma wangu basi ningemfanya Abuubakari kuwa kipenzi wa ndani, Fahamuni kuwa hakika wale waliyokuwa kabla yenu waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti, Tambueni kuwa, msiyafanye makaburi kuwa Misikiti, kwani hakika mimi ninakukatazeni na hilo".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Anazungumza rehema na Amani ziwe juu yake kabla ya kifo chake, kwa umma wake kwa mazungumzo muhimu, akaeleza nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu nakuwa imefikia daraja nyingi za mapenzi kama alivyoipata Ibrahim Amani iwe juu yake, na kwaajili hiyo akakanusha kuwa na kipenzi mwingine wa ndani zaidi ya Mwenyezi Mungu; kwasababu moyo wake umejaa mapenzi yake na kumtukuza kwake na kumjua kwake, hivyo haufunguki kwa yeyote, na mapenzi ya ndani katika moyo wa kiumbe hayawi ila kwa mmoja, na lau kama angekuwa na kipenzi wa ndani katika viumbe basi angekuwa Abuubakari Swiddiq radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, nayo ni ishara juu ya ubora wa Abuubakari na kumfanya kuwa kiongozi baada yake, kisha akaeleza kuchupa mipaka kwa Mayahudi na Wakristo katika makaburi ya Manabii wao mpaka wakayageuza kuwa viabudiwa vya kishirikina, na akaukataza umma wake wasifanye mfano wa vitendo vyao, na wakristo hawana ispokuwa Nabii mmoja naye ni Isa (Yesu), lakini wanaamini kuwa anakaburi ardhini, na usahihi nikuwa Isa Amani iwe juu yake alinyanyuliwa na wala hakusulubiwa na wala hakuzikwa.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani Pashto
Kuonyesha Tarjama

من فوائد الحديث

  1. Kuthibitisha mapenzi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yale yanayoendana na Utukufu wake.
  2. Ubora wa vipenzi wawili wa ndani: Muhammadi na Ibrahim- Amani iwe juu yao-.
  3. Ubora wa Abuubakari Swiddiq, nakuwa yeye ndiye mbora katika umma mzima kwa ujumla.
  4. Nikuwa hiyo ni ishara juu ya utawala wa Abuubakari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
  5. Kuthibitika kwa mapenzi ya ndani ya Mtume rehema na Amani ziwe juu yake kwa Mwenyezi Mungu.
  6. Nikuwa kujenga misikiti juu ya makaburi ni utaratibu wa umma zilizotangulia.
  7. katazo la kuyafanya makaburi kuwa maeneo ya ibada panaposwaliwa hapo au kupaelekea, na pakajengwa juu yake misikiti au vikuba (vibanda), kwa tahadhari ya kuingia katika ushirikina kwasababu ya hilo.
  8. Kuziba miyanya inayoweza kupelekea katika ushirikina.