عن النعمان بن بشير رضي الله عنهما مرفوعًا: «مَثَلُ القَائِم في حُدُود الله والوَاقِعِ فيها كمَثَل قَوم اسْتَهَمُوا عَلَى سَفِينَة فصارَ بعضُهم أَعلاهَا وبعضُهم أسفَلَها، وكان الذين في أسفَلِها إِذَا اسْتَقَوا مِنَ الماءِ مَرُّوا على من فَوقهِم، فَقَالُوا: لَو أَنَّا خَرَقْنَا فِي نَصِيبِنَا خَرْقاً وَلَم نُؤذِ مَنْ فَوقَنَا، فَإِنْ تَرَكُوهُم وَمَا أَرَادُوا هَلَكُوا جَمِيعاً، وَإِنْ أَخَذُوا عَلَى أَيدِيهِم نَجَوا وَنَجَوا جَمِيعاً».
[صحيح] - [رواه البخاري]
المزيــد ...

Kutoka kwa Nu'man bin Bashiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina) wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, wakasema: Lau kama tungetoboa katika sehemu yetu kitobo wala tusingewaudhi walioko juu yetu, ikiwa watawaacha watekeleze walilolikusudia wataangamia wote, na ikiwa watawashika na kuwazuia wataokoka na wataokoka wote".
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Ufafanuzi

Hadithi ya Nu'mani bin Bashiri Al Answariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- iko katika mlango wa kuamrisha mema na kukataza mabaya, kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye amesema: "Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake" Aliyesimama ndani yake yaani: ni yule aliyenyooka katika dini ya Mwenyezi Mungu akatekeleza mambo yote ya wajibu, na akaacha maharamisho, na mwenye kuingia ndani yake: Yaani: katika mipaka ya Mwenyezi Mungu, yaani: mwenye kufanya makatazo na kuacha maamrisho."Ni kama mfano wa watu walioshauriana katika kupanda safina" yaani waliopiga kura, ni nani kati yao atakayekuwa juu? "wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji" Yaani wanapotaka maji; ili wanywe "Wanapita kwa wale walioko juu yao", Yaani wale walioko juu yao; kwasababu maji hakuna anayeweza kuyachota isipokuwa aliye juu."Wakasema: lau kama tungelitoboa katika sehemu yetu", Yaani laiti tukitoboa kitobo sehemu yetu ili tuchote maji hapo, ili tusiwaudhi walioko juu yetu, hivyo ndivyo walivyofikiria na wakataka na wakatamani. Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Ikiwa watawaacha na hicho walichokitaka wataangamia wote"; kwasababu wao atakapotoboa kitobo chini ya safina maji yataingia kisha safina nzima itazama."Na ikiwa watawashika na kuwazuia" Na wakawazuia na hilo "watasalimika na watasalimika wote" Yaani watasalimika hawa na wale. Na mfano huu alioupiga Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni miongoni mwa mifano ambayo ina kiwango cha juu na maana ya juu, hivyo watu katika dini ya Mwenyezi Mungu ni kama wale waliopanda safina katika wimbi la mto, wakitupwa na mawimbi, na ni lazima wanapokuwa wengi baadhi yao wawe juu na baadhi yao wawe chini, ili ulingane uzito wa safina na ili wasibanane, na ndani yake nikuwa safina hii ambayo wanashirikiana kati ya hawa watu atakapotaka mmoja wao kuiharibu basi wanalazimika kumshika na kumzuia, ili wasalimike wote, wasipofanya hivyo wataangamia wote, hivyo ndivyo ilivyo dini ya Mwenyezi Mungu, ikiwa watawazuia wale wenye akili na maarifa ya dini wale wajinga na wapumbavu watasalimika wote, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na ogopeni fitina (mtihani) ambao hauwapati wale waliodhulumu pekee, na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu".

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama