+ -

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِنَّ مِنْ أَعْظَمِ الجِهَادِ كَلِمَةَ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ».

[حسن لغيره] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد] - [سنن الترمذي: 2174]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hakika katika Jihadi kubwa ni kusema neno la uadilifu kwa kiongozi dhalimu".

[Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyingine] - - [سنن الترمذي - 2174]

Ufafanuzi

Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa moja ya aina kubwa ya jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na yenye manufaa makubwa ni neno la uadilifu na ukweli mbele ya mtawala au mfalme dhalimu, kwa sababu ni kuifanyia kazi sheria ya kuamrisha mema na kukataza maovu, iwe kwa maneno au maandishi au vitendo, au kitu chochote kile, ili kuleta manufaa na kuzuia maovu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الليتوانية الدرية الرومانية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuamrisha mema na kukataza maovu ni katika Jihadi.
  2. Kumnasihi kiongozi ni katika Jihadi kubwa, lakini ni lazima iwe kwa elimu na hekima na kuwa na uhakika.
  3. Amesema Imam Al-Khattabi: Hii imekuwa jihadi bora kabisa kwa sababu anaye pigana na adui husitasita baina ya kuwa na matumaini na khofu, hajui atashinda au atashindwa, na kiongozi ana mamlaka mkononi mwake, hivyo ikiwa atasema kweli na akamuamrisha mema atakuwa kajitia katika hatari, na kaiweka nafsi yake katika maangamivu, hivyo ikawa ni aina bora ya jihadi kwa sababu ya kushinda khofu, na imesemwa kuwa: Imekuwa ni Jihadi bora; Kwa sababu ikiwa mtawala atachukua neno lake, faida inaweza kuenea kwa idadi kubwa ya watu, na masilahi yatapatikana.