عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه عن النبيِّ -صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم- قَالَ: «إن الدنيا حُلْوَةٌ خَضِرَةٌ، وإن الله مُسْتَخْلِفُكُمْ فيها فينظرَ كيف تعملون، فاتقوا الدنيا واتقوا النساء؛ فإن أول فتنة بني إسرائيل كانت في النساء».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake; kwani hakika fitina ya kwanza ya wana wa Israeli ilikuwa kwa wanawake".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Ameifananisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- dunia na tunda tamu la kijani, kwasababu ya kuhamasisha ndani yake na kuielekea, na akaeleza kuwa Mwenyezi Mungu ametufanya sisi kuwa watawala, baadhi yetu wanawaachia wengine ndani yake; kwani haijafika dunia hii kwa watu isipokuwa baada ya wengine,basi anatazama Mwenyezi Mungu Mtukufu ni jinsi gani tutafanya ndani yake, je tutatekeleza utiifu wake au la. Kisha akatuamrisha Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- tutahadhari na fitina ya dunia na tusidanganyike nayo, na tukaacha maamrisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuyaepuka makatazo yake. Na ilipoonekana kuwa wanawake wana fungu kubwa katika fitina hii, akatutahadharisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya hatari ya kufitinika nao hata kama hii inaingia katika fitina ya dunia; na akaeleza kuwa fitina ya wana wa Israeli sababu yake ilikuwa ni wanawake, na kwasababu yao wameangamia waheshimiwa wengi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama