+ -

عن عمران بن حصين رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رسولُ اللَّه -صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم-: «الحَيَاءُ لاَ يَأْتِي إِلاَّ بِخَيرٍ». وفي رواية : «الحَيَاءُ خَيرٌ كُلُّهٌ» أو قال: «الحَيَاءُ كُلُّهُ خَيرٌ».
[صحيح] - [الرواية الأولى: متفق عليها. الرواية الثانية والثالثة: رواها مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Imrani bin Huswain -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Haya (Aibu) haiji ila kwa kheri". na katika riwaya nyingine: "Haya ni kheri yote" Au alisema: "Haya yote ni kheri".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

Ufafanuzi

Haya(Aibu) ni sifa iliyoko katika nafsi inayomsukuma mtu kufanya mazuri au yanayopendeza, na kuacha yanayochafua na kuharibu, na ndio maana haiji isipokuwa kwa kheri, na sababu ya kuja kwa hadithi hii nikuwa mtu mmoja alikuwa akimnasihi ndugu yake kuhusu haya, na akimkataza kuhusu haya, Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema kumwambia maneno haya.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama