+ -

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضيَ اللهُ عنهما أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ:
«اللهُمَّ لَكَ أَسْلَمْتُ، وَبِكَ آمَنْتُ، وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ، وَإِلَيْكَ أَنَبْتُ، وَبِكَ خَاصَمْتُ، اللهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِعِزَّتِكَ، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ أَنْ تُضِلَّنِي، أَنْتَ الْحَيُّ الَّذِي لَا يَمُوتُ، وَالْجِنُّ وَالْإِنْسُ يَمُوتُونَ».

[صحيح] - [متفق عليه، وهذا لفظ مسلم ورواه البخاري مختصرًا] - [صحيح مسلم: 2717]
المزيــد ...

Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema:
"Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa".

[Sahihi] - - [صحيح مسلم - 2717]

Ufafanuzi

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako nimejisalimisha" na nimenyenyekea, "na kwako nimeamini" na nimesadikisha na nimekiri, "Na juu yako nimetegemea" na nimekabidhi na nimetegemea, "na kwako nimetubia" na nimerejea na nimekuja, "na kwako ninapambana" na ninajibizana kwa hoja na maadui zako, "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda kwako" Ninajiegemeza, "kwa utukufu wako" na ngome yako na ushindi wako, "hapana mola wa haki isipokuwa wewe" na wala hakuna muabudiwa wa haki zaidi yako, "unipoteze" kutoka katika uongofu na taufiki ya kupata radhi zako, "Wewe ndiye uliye hai ambaye hafi" na wala hamaliziki, "na majini na watu wote wanakufa".

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sheria ya kutanguliza sifa katika kila mahitaji.
  2. Ulazima wa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake na kuomba hifadhi kutoka kwake; kwa sababu yeye ndiye mwenye kusifika kwa sifa kamilifu, basi yeye peke yake yake ndiye mwenye kutegemewa, na viumbe wote hawajiwezi na mwisho wao ni kifo, hivyo wao hawastahiki kutegemewa.
  3. Kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika dua kwa maneno haya yaliyokusanya kila kitu, na yenye kuzuia kingenecho kuingia humo, yanayoelezea kwa imani ya kweli na yakini ya kiwango cha juu.
  4. Amesema As-Sa'diy: Kauli yake: "Wewe ndiye uliye hai" Yaani: Wewe pekee ndiye unayestahiki kuombwa kinga na si mwingine zaidi yako.