عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنين رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ:
مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُسْتَجْمِعًا قَطُّ ضَاحِكًا، حَتَّى أَرَى مِنْهُ لَهَوَاتِهِ، إِنَّمَا كَانَ يَتَبَسَّمُ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6092]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, amesema:
Sikumuona Mtume -rehema amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6092]
Alieleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema amani ziwe juu yake alikuwa hapitilizi kucheka mpaka kionekane kilimi chake, nacho ni kinyama kinachoning'inia juu ya koo, bali alikuwa akitabasam.