عن عبادة بن الصامت رضي الله عنه قال: بَايَعْنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم على السَّمع والطَّاعَة في العُسْر واليُسْر، والمَنْشَطِ والمَكْرَه، وعلَى أَثَرَةٍ عَلَينا، وعلى أَن لاَ نُنَازِعَ الأَمْر أَهْلَه إِلاَّ أَن تَرَوْا كُفْراً بَوَاحاً عِندَكُم مِن الله تَعَالى فِيه بُرهَان، وعلى أن نقول بالحقِّ أينَما كُنَّا، لا نخافُ فِي الله لَوْمَةَ لاَئِمٍ.
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ubada bin Swamit- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Tulimuunga mkono Mtume rehema na Amani zimfikie- juu ya usikivu na Utii katika ugumu na wepesi, na katika raha na karaha, na hata kwa kujinyima sisi, nakuwa tusizozane na watu katika jambo wanalostahiki ispokuwa mkiona ukafiri wa wazi na mkawa kutoka kwa Mwenyezi Mungu mna hoja juu yake, nakuwa tuseme ukweli mahala popote tutakapokuwa, Hatuogopi kwa Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulaumu.
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

(Tulimuunga mkono) Yaani walimuunga mkono maswahaba- radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Mtume rehema na Amani ziwe juu yake- Juu ya usikivu na utii; kwasababu Mwenyezi Mungu Mtukufu- amesema: "Enyi mlioamini mtiini Mwenyezi Mungu na mumtii Mtume na wale wenye amri miongoni mwenu" na baada yake rehema na Amani zimfikie- wenye Amri nao wako makundi mawili: Wanachuoni na viongozi, lakini wanachuoni wao ni wasimamizi wa mambo katika elimu na kubainisha, ama viongozi wao ni wasimamizi wa mambo katika utekelezaji na utawala. Anasema: Tulimuunga mkono juu ya usikivu na utii, na kauli yake: "katika ugumu na wepesi" yaani sawasawa raia wawe na hali ngumu ya kiuchumi au iwe nyepesi, ni wajibu kwa raia wote matajiri kwa masikini kuwatii wasimamizi wa mambo yao katika raha na karaha, yaani sawasawa raia wawe wanalichukia hilo kwakuwa wameamrishwa lile wanalolichukia wala nafsi zao hazilitaki, au wawe na furaha kwakuwa wameamrishwa linalonasibiana nao na kuendana nao. "Na hata kwa kujinyima sisi" Kujinyima yaani kwa kukupendelea kuliko nafsi zetu, yaani lau kama viongozi wangekuwa wanajipendelea juu ya mali za umma juu ya raia au wengineo, katika vile ambavyo nafsi zao zinavipupia na wanawanyima wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa kuwaongoza, pia bado ni wajibu kutii na kusikiliza kisha akasema "Na tusizozane na watu katika jambo wanalostahiki" Yaani tusizozane na viongozi kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu kwetu sisi, tuchukue amri kutoka kwao, kwasababu mzozo huu hupelekea shari nyingi, na fitina kubwa, na kuwatenganisha waislamu, na hakuna kilichobomoa jambo la uislamu ispokuwa ni kuzozania uongozi kwa viongozi, tangu zama za Othmani radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mpaka zama zetu hizi. Akasema: Ispokuwa mkiona ukafiri wa wazi mnayo hoja yawazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu" Hizi ni sharti nne, tutakapoliona hili na sharti nne zikatimia hapo inaruhusiwa kuzozania jambo hilo kwa watu wake (viongozi), na tutajaribu kuwaondoa katika usimamizi wa mambo, na sharti hizo ni: Ya kwanza: Mpaka muone, ni lazima kujua, ama ikiwa ilimradi dhana tu, hapo haifai kujitoa kwa viongozi. Ya pili: Tujue kuwa kuna ukafiri na sio uovu, kwa namna yoyote watakayofanya viongozi haifai kujitoa kwao, hata wakinywa pombe, wakazini, wakadhulumu watu, haifai kujitoa kwao, lakini tukiona ukafiri wa wazi hapo unakuwa dhahiri. Ya tatu: Ukafiri wa wazi: Na hii maana yake ni ukafiri wa dhahiri, yaani kitu kilicho bayana, ama yanayokuwa na maana zaidi ya moja haifai kujitoa kwao, Yaani kwa mfano tuchukulie kuwa wamefanya kitu ambacho sisi tunaona ni ukafiri, lakini kunauwezekano kuwa wakati mwingine isiwe ni ukafiri, hapo haifai kujitoa kwao, na tutasimamia waliyoyasimamia, lakini ikiwa ni wa wazi dhahiri, mfano: kama ikiitakidi uhalali wa ulevi na uzinifu. Ya nne: "mnayo hoja kutoka kwa Mwenyezi Mungu": Yaani tuna dalili ya wazi yakuwa hili ni ukafiri,Na ikiwa dalili tuliyonayo ni dhaifu katika kuthibiti kwake, au nidhaifu katika kuitolea ushahidi, hapo haifai kujitoa kwao, kwasababu kujitoa kuna shari nyingi sana na ni madhara makubwa. na tukiliona hili mfano haitofaa kuzozana mpaka tuwe na uwezo wa kuliondoa, ikiwa raia hawana uwezo wa kuliondoa basi haifai kuzozana, kwasababu huenda raia wakizozana naye na hali yakuwa hawana uwezo unaopelekea kubakisha kizuri na utimilifu wa kumteka. Basi sharti ima ni za kujuzisha (kuonyesha kuwa inafaa) au ni wajibu, uwajibu wa kujitoa kwa kiongozi, lakini kwa sharti kuwe na uwezo, ikiwa kama uwezo hautokuwepo, haitofaa kujitoa; kwasababu hilo litakuwa ni katika kuitia nafsi katika maangamivu; kwasababu hakuna faida ya kujitoa.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani Pashto
Kuonyesha Tarjama

من فوائد الحديث

  1. Kuhimizwa juu ya usikivu na utii kwa wasimamizi wa mambo (viongozi) katika waislamu katika mambo yasiyokuwa maasi.
  2. Matunda ya utiifu katika yote yaliyotajwa katika hadithi nikuwa pamoja neno la waislamu (umoja wao) na kuachana na tofauti katika safu yao.
  3. Kutozozana na viongozi ispokuwa utakapodhihiri kwao ukafiri uliothibitika, hapo italazimu kuwakemea na kuinusuru haki kwa namna yoyote ile itakayokuwa kujitoa muhanga.
  4. Uharamu wa kujitoa kwa viongozi na kupigana nao, kwa makubaliano ya wanachuoni, hata kama watakuwa waovu, kwasababu katika kujitoa kwao kuna madhara makubwa kuliko huo uovu wao, hivyo atafanya madhara yenye nafuu kati ya madhara mawili.
  5. Kumuunga mkono kiongozi mkuu hakuwi ispokuwa katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  6. Kumtii kiongozi Mkuu katika mambo mema ni lazima katika furaha na karaha na uzito na wepesi, hata kama atakwenda kinyume na matamanio ya nafsi.
  7. Kuheshimu haki ya viongozi, nakuwa ni wajibu kwa watu kuwatii katika wepesi na uzito, na furaha na karaha, na kuwapendelea yale wanayo yapendelea.