عَنْ عُثْمَانَ الشَّحَّامِ، قَالَ: انْطَلَقْتُ أَنَا وَفَرْقَدٌ السَّبَخِيُّ إِلَى مُسْلِمِ بْنِ أَبِي بَكْرَةَ وَهُوَ فِي أَرْضِهِ، فَدَخَلْنَا عَلَيْهِ فَقُلْنَا: هَلْ سَمِعْتَ أَبَاكَ يُحَدِّثُ فِي الْفِتَنِ حَدِيثًا؟ قَالَ: نَعَمْ، سَمِعْتُ أَبَا بَكْرَةَ رضي الله عنه يُحَدِّثُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِنَّهَا سَتَكُونُ فِتَنٌ، أَلَا ثُمَّ تَكُونُ فِتْنَةٌ الْقَاعِدُ فِيهَا خَيْرٌ مِنَ الْمَاشِي فِيهَا، وَالْمَاشِي فِيهَا خَيْرٌ مِنَ السَّاعِي إِلَيْهَا، أَلَا فَإِذَا نَزَلَتْ أَوْ وَقَعَتْ فَمَنْ كَانَ لَهُ إِبِلٌ فَلْيَلْحَقْ بِإِبِلِهِ، وَمَنْ كَانَتْ لَهُ غَنَمٌ فَلْيَلْحَقْ بِغَنَمِهِ، وَمَنْ كَانَتْ لَهُ أَرْضٌ فَلْيَلْحَقْ بِأَرْضِهِ»، قَالَ فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ أَرَأَيْتَ مَنْ لَمْ يَكُنْ لَهُ إِبِلٌ وَلَا غَنَمٌ وَلَا أَرْضٌ؟ قَالَ: «يَعْمِدُ إِلَى سَيْفِهِ فَيَدُقُّ عَلَى حَدِّهِ بِحَجَرٍ، ثُمَّ لِيَنْجُ إِنِ اسْتَطَاعَ النَّجَاءَ، اللهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ؟ اللهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ؟ اللهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ؟»، قَالَ: فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ أَرَأَيْتَ إِنْ أُكْرِهْتُ حَتَّى يُنْطَلَقَ بِي إِلَى أَحَدِ الصَّفَّيْنِ، أَوْ إِحْدَى الْفِئَتَيْنِ، فَضَرَبَنِي رَجُلٌ بِسَيْفِهِ، أَوْ يَجِيءُ سَهْمٌ فَيَقْتُلُنِي؟ قَالَ: «يَبُوءُ بِإِثْمِهِ وَإِثْمِكَ، وَيَكُونُ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2887]
المزيــد ...
Kutoka kwa Othman As Shaham, amesema:Niliondoka mimi pamoja na Farqad As Sabakhi kwenda kwa Muslim bin Abii Bakara naye akiwa katika mji wake, tukaingia kwake na tukasema: Hivi uliwahi kumsikia baba yako akisimulia hadithi yoyote kuhusu fitina? Akasema: Ndiyo, Nilimsikia Abuu Bakra radhi za Allah ziwe juu yake akihadithia, akasema: Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Hakika zitatokea fitina, kisha tambueni kuwa fitina ya aliyekaa ndani inanafuu kuliko anayetembea, na anayetembea ndani yake inanafuu kuliko anayeikimbilia, tambueni itakapoteremka au ikatokea basi atakayekuwa na ngamia basi na amfuate ngamia wake, na atakayekuwa na mbuzi basi na amfuate mbuzi wake, na atakayekuwa na ardhi basi na aende katika ardhi yake", anasema, akasema mtu mmoja: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje ikiwa mtu hana ngamia wala mbuzi wala ardhi? Akasema: "Basi achukue panga lake na apige upande wa makali yake katika jiwe, kisha aokoke akiweza kuokoka, ewe Allah je nimefikisha? ewe Allah je nimefikisha? ewe Allah je nimefikisha?" Akasema: Akasema mtu mmoja: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje endapo nitalazimishwa mpaka nikapelekwa katika moja kati ya safu mbili, au moja kati ya makundi mawili, mtu mmoja akanipiga kwa panga lake, au ukanilenga mshale ukaniua? Akasema: "Yeye ndiye atakayebeba dhambi zake na dhambi zako, na atakuwa miongoni mwa watu wa motoni".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2887]
Othman Ash Shaham na Farqad As-Sabakhi walimuuliza Muslim mtoto wa Swahaba mtukufu Abuubakra radhi za Allah ziwe juu yake: Je alisikia kutoka kwa baba yake hadithi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika fitina na vita itakayotokea baina ya waislamu? Akasema: Naam, alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba itatokea fitina baada ya kifo chake, na fitina hii aliyekaa na kughafilika nayo ni bora kuliko anayetembea ndani yake, na anaitafuta pasina kujua, na anayetembea ndani yake ni bora kuliko anayekwenda mbio kuiendea na kuitafuta na kushiriki ndani yake. Kisha akaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake itakayeshuka na kufika fitina katika zama zake na kwake kukapatikana upenyo atakaokimbilia; atakayekuwa na ngamia anayechunga basi aifuate ngamia yake, na atakayekuwa na mbuzi anayechunga basi amfuate mbuzi wake, na atakayekuwa na ardhi na shamba basi aende shambani kwake. Bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hivi wasemaje kwa mtu ambaye hatokuwa na makimbilio kama ngamia wala mbuzi wala shamba? Akasema: Basi aende akachukue silaha yake aipige na ailainishe, kisha akimbie na ajinusuru yeye na mwanaye ikiwa ataweza kuokoka. Kisha akataka ushuhuda rehema na amani ziwe juu yake mara tatu, akasema: Ewe Allah je, nimefikisha? Ewe Allah je nimefikisha? Ewe Allah je nimefikisha?. Bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje ikiwa nitalazimishwa kushiriki pamoja na safu moja, au moja kati ya makundi mawili, akanipiga mtu kwa panga lake, au mshale ukanilenga ukaniuwa?. Akasema: Atarudi na madhambi yake na madhambi ya aliyemuuwa, na siku ya Kiyama atakuwa miongoni mwa watu wa motoni.