عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: «من خرج من الطاعة، وفارق الجماعة فمات، مات مِيتَةً جاهلية، ومن قاتل تحت راية عِمِّيَّة يغضب لِعَصَبَة، أو يدعو إلى عَصَبَة، أو ينصر عَصَبَة، فقتل، فَقِتْلَة جاهلية، ومن خرج على أمتي، يضرب برها وفاجرها، ولا يَتَحَاشَى من مؤمنها، ولا يفي لذي عهد عهده، فليس مني ولست منه»،
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye amesema: "Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga, na atakayepigana chini ya bendera kibubusa anachukia kwasababu ya ndugu zake, au akahamasisha katika (kupendelea kwasababu ya) udugu, au ana nusuru udugu, akauwawa, basi hicho ni kifo cha zama za ujinga, na atakayejitoa katika umma wangu, akimpiga mwema wake na muovu wake, na wala hajali muumini wake, na wala hamtimizii mwenye ahadi ahadi yake, basi huyo si miongoni mwangu na mimi si miongoni mwake".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Maana ya hadithi hii nikuwa: atakayesambaratisha kundi la watu ambao wamekubaliana juu ya kumtii kiongozi, nguvu yao na kauli yao kwake ikawa ni moja, na akawazingira kwa maadui wao, na akajitoa katika utiifu wa kiongozi wa waislamu, na akafa akiwa katika hali hiyo, basi atakuwa amekufa kama vifo vya watu wa zama za ujinga, kiasi kwamba kwao ni vurugu wala hawana kiongozi, na atakayepigana chini ya bendera ambayo jambo lake halijulikani, hauko wazi muelekeo wake, kama watu kupigana kwasababu za ubaguzi na ukabila, na anachukia kwasababu ya ubaguzi na anashawishi watu katika ubaguzi au ana nusuru ubaguzi, Na maana yake nikuwa yeye anapigana kwasababu ya matamanio ya nafsi yake na hasira zake na kwa kutetea watu wake na matamanio yake. Na atakayetoka katika umma akimpiga mwema na muovu, muumini na alipewa hifadhi ya kuishi katika mji wake, na aliyechukua makubaliano ya kuishi katika miji ya kiislamu kwa kulipa kodi, na wala hajali anachokifanya ndani yake, na wala haogopi mwisho wake na adhabu zake, basi mtu huyu amejiepusha naye Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuwatii wenye mamlaka ni wajibu katika yale yasiyokuwa ya kumuasi Mwenyezi Mungu -Mtukufu-.
  2. Kuna tahadhari kubwa kwa mwenye kujitoa kwa waislamu, na katika kumtii kiongozi, na akasambaratisha umoja wa waislamu, ikiwa atakufa katika hali hii, basi atakuwa amekufa katika njia ya watu wa zama za ujinga.
  3. Katika hadithi kuna ushahidi kuwa atakapojitoa mtu katika jamaa, na akawa hajatoka dhidi yao, na akawa hajawapiga, basi hatutakiwi kumpiga kwaajili ya kumrudisha katika jamaa na amtii kiongozi kwa mambo ya batili, bali tunamuacha na jambo lake.
  4. katika utiifu na kushikamana na umoja kuna kheri nyingi, na amani na utulivu, na kutengemaa kwa hali.