عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ أُمِّ المُؤمنين رضي الله عنها: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ:
«سَتَكُونُ أُمَرَاءُ فَتَعْرِفُونَ وَتُنْكِرُونَ، فَمَنْ عَرَفَ بَرِئَ، وَمَنْ أَنْكَرَ سَلِمَ، وَلَكِنْ مَنْ رَضِيَ وَتَابَعَ» قَالُوا: أَفَلَا نُقَاتِلُهُمْ؟ قَالَ: «لَا، مَا صَلَّوْا».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1854]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Watakuja watawala, mtayajua baadhi ya matendo yao kuwa yanakwenda sawa na sheria, na mengine mtayakemea (kwa kuwa yako nje ya sheria) atakayelijua hilo ataepukana na dhima, na atakayekemea atasalimika, lakini atakayeridhia na akawafuata" Wakasema: Kwa nini tusiwapige vita? Akasema: "Hapana, (Msifanye hivyo) madam ni waislamu na wanasimamisha swala".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1854]
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa tutatawaliwa na viongozi ambao tutayajua baadhi ya matendo yao kuwa yako sawa na yale yanayofahamika ndani ya sheria; na tutayakemea baadhi yake kwa kuwa kwake kinyume na sheria, Atakayechukia moyoni mwake na akawa hakuweza kukemea; basi atakuwa kaondoa dhima ya kupata dhambi na unafiki, Na atakayeweza kukemea kwa mkono au ulimi akawakemea kwa hilo basi atakuwa kasalimika na maasi na kushiriki katika maasi, Lakini atakayeridhia matendo yao na akawafuata ataangamia kama walivyoangamia.
Kisha wakamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kwa nini tusiwapige vita viongozi ambao wanasifa kama hizi? Akawakataza wasifanye hivyo, na akasema: Hapana, msifanye hivyo madama wanasimamisha swala kwenu nyinyi.