عن مَعقِلِ بن يَسار المُزَنِيّ رضي الله عنه قال: إني سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:
«مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ، إِلَّا حَرَّمَ اللهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 142]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ma'akali bin Yasaari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Hakika mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Hakuna mja yeyote atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia, akafa siku atakayokufa hali yakuwa aliwafanyia udanganyifu raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia pepo".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 142]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila mtu ambaye Mwenyezi Mungu atamfanya kuwa ni msimamizi au kiongozi kwa watu, sawa sawa uwe ni uongozi wa umma, kama Raisi au usimamizi wa sekta binafsi kama mtu katika nyumba yake na mwanamke katika nyumba yake, akafanya uzembe kutekeleza haki za raia wake, na akawafanyia udanganyifu na wala hakuwanasihi, akapoteza haki zao za kidini na kidunia, huyu atakuwa kastahiki adhabu hii kali.