عَنْ أَبِي ذَرٍّ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«يَا أَبَا ذَرٍّ إِذَا طَبَخْتَ مَرَقَةً فَأَكْثِرْ مَاءَهَا، وَتَعَاهَدْ جِيرَانَكَ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2625]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Ewe Abuu Dhari utakapopika mchuzi basi zidisha maji yake, na umkumbuke jirani yako".

[Sahihi] - [Imepokelewa Imamu Muslim] - [Swahiih Muslim - 2625]

Ufafanuzi

Alimhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Abuu Dhari Al-Ghifaari radhi za Allah ziwe juu yake atakapopika mchuzi basi azidishe maji yake na mchuzi wake, na amkumbuke na amtafute jirani yake.

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kuwa na mahusiano mazuri na jirani.
  2. Sunna ya kupeana zawadi kati ya majirani wawili; kwa sababu hilo linaleta mapenzi na mahaba, na kunakuwa na mkazo zaidi kupeana zawadi huku pindi chakula kinapokuwa na harufu nzuri, na ikajulikana hali ya jirani.
  3. Himizo la kutenda wema na kila kinachowezekana hata kikiwa kidogo, na kuingiza furaha kwa waislamu.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (36)