عن ابن عمر رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«مَا زَالَ يُوصِينِي جِبْرِيلُ بِالْجَارِ، حَتَّى ظَنَنْتُ أَنَّهُ سَيُوَرِّثُهُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6014]
المزيــد ...
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakuacha Jibrili kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhania kuwa atamrithisha".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6014]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Jibrili akikariri kwake na akimuamrisha kumjali jirani, ambaye ni wakaribu kimakazi, sawa awe muislamu au kafiri, na sawa sawa awe ndugu wa karibu wa mbali, kwa kuhifadhi haki zake na kutomuudhi, na kumtendea wema na kuvumulia kero zake, mpaka akadhania -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kule kuitukuza kwake haki ya jirani na kitendo cha Jibrili kulirudiarudia hilo kwamba utakuja kuteremsha wahyi wa kumpa katika mali zake jirani yake atakayebakia baada ya kifo chake.