عَنْ أَبِي شُرَيْحٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ، وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ، وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ»، قِيلَ: وَمَنْ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «الَّذِي لاَ يَأْمَنُ جَارُهُ بَوَايِقَهُ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6016]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Shuraihi radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema:
"Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6016]
Aliapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akasisitiza kiapo chake mara tatu, akasema: Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Maswahaba wakamuuliza: Na ni nani ambaye hawezi kuamini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ambaye jirani anahofia usaliti wake na dhulma zake na shari zake.