عن ابْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهُما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«أَيُّمَا امْرِئٍ قَالَ لِأَخِيهِ: يَا كَافِرُ، فَقَدْ بَاءَ بِهَا أَحَدُهُمَا، إِنْ كَانَ كَمَا قَالَ، وَإِلَّا رَجَعَتْ عَلَيْهِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 60]
المزيــد ...
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mtu yeyote atakayesema kumwambia ndugu yake: Ewe kafiri, basi utampata mmoja katika ya hao wawili, ikiwa atakuwa kama alivyosema (litathibiti hilo), na kama si hivyo utarejea kwake".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 60]
Amemtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kusema kumwambia ndugu yake muislamu: Ewe kafiri, basi atakuwa kastahiki neno kafiri mmoja wao, na ikiwa ni kweli kama alivyosema (utamthibitikia), na kama si kweli ukafiri utarejea kwa msemaji aliyesema kumwambia ndugu yake.