+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قِيلَ: يَا رَسُولَ اللهِ ادْعُ عَلَى المُشْرِكِينَ قَالَ:
«إِنِّي لَمْ أُبْعَثْ لَعَّانًا، وَإِنَّمَا بُعِثْتُ رَحْمَةً».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2599]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Palisemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu waombee dua mbaya washirikina, akasema:
"Hakika mimi sikutumwa kuwa mtoa laana, bali nilitumwa kuwa huruma".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2599]

Ufafanuzi

Alitakwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake awaombee washirikina dua mbaya kwa Mwenyezi Mungu, akasema: Hakika mimi sikuagizwa na Mwenyezi Mungu na sikutumwa kuwa mtoa laana na kuwaombea watu kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na niwakatie heri, mimi sikutumwa kwa hayo, bali nilitumwa niwe sababu ya heri na rehema kwa watu wote, na kwa waumini hasa.

Katika Faida za Hadithi

  1. Ukamilifu wa tabia zake rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Umuhimu wa kuusafisha ulimi kutokana na laana kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Hapa kuna katazo la kutoa laana.
  4. Himizo la kuwahurumia watu.
Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kikurdi Kireno Thai Kiassam الهولندية الدرية المجرية الجورجية المقدونية الخميرية
Kuonyesha Tarjama