عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: كان رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا عطس وضع يده أو ثوبه على فيه، وخفض -أو غض- بها صوته،
شك الراوي.
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وأحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza -au anazuia- sauti yake, hapa kuna shaka kwa mpokezi.
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy
Imeonyesha hadithi juu ya adabu miongoni mwa adabu zinazohusiana na chafya, ni sunna kwa mwenye kupiga chafya asipitilize katika kupiga chafya na asinyanyue sauti yake, bali aipunguze na afunike uso wake ikiwezekana.