عن عائشة رضي الله عنها قالت: كَانَ كَلاَمُ رَسُولِ الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- كَلاَمًا فَصلاً يَفْهَمُهُ كُلُّ مَنْ يَسْمَعُهُ.
[حسن] - [رواه أبو داود واللفظ له، والتُرمذي والنسائي وأحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Yalikuwa maneno ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni maneno ya wazi anayaelewa kila mwenye kuyasikia.
Ni nzuri - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy

Ufafanuzi

Hadithi ya Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alisema kuwa: Hakika Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yalikuwa wazi maneno, maana yake nikuwa yalikuwa yamepambanuka, hachanganyi herufi baadhi yake kwa baadhi, wala maneno baadhi yake kwa baadhi, yanaeleweka yako wazi kwa kila mwenye kuyasikia hakuna kufungana ndani yake wala kurefusha, hata wangetaka wenye kuhesabu kuyahesabu basi wangeyahesabu, kwasababu ya utaratibu wake mkubwa katika maneno -Rehema na Amani ziwe juu yake-; hii ni kwasababu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kapewa mkusanyiko wa maneno yenye kuweza kumaanisha vitu vingi, na yakawa mafupi sana kwake maneno, na mkusanyiko wa maneno ni kukusanya maana nyingi katika matamshi machache. Na hivi ndivyo inavyotakiwa mtu maneno yake yasiwe ni yenye kuingiliana kiasi kwamba yakafichikana kwa msikilizaji; kwasababu makusudio ya kuzungumza ni kumuelewesha mwenye kuzungumzishwa, kila yanavyozidi kuwa karibu kueleweka ndivyo inavyokuwa bora na vizuri zaidi. Kisha inampasa kila mtu atakapotumia njia hii, yaani atakapofanya maneno yake kuwa vipengele vya wazi, na akayarudia mara tatu kwa yule ambaye hajaelewa, inampasa avute hisia katika hili kuwa yeye anamfuata Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ili aweze kupata kupitia hili thawabu na amfahamishe ndugu yake muislamu. Na hivyo hivyo sunna zote weka akilini mwako kuwa ndani yake unamfuata Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ili kuthibiti kwako kumfuata Mtume na thawabu pia.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama