عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال:
كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَحْسَنَ النَّاسِ خُلُقًا.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2310]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mtu mwenye tabia nzuri mno kuliko watu wote.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2310]
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa na tabia zilizokamilika kuliko watu wote, na mtu wa mbele katika tabia njema na mambo mazuri, kama maneno mazuri, na kufanya heri, na uso mkunjufu, na kujizuia na maudhi na kuyavumilia kutoka kwa wengine.