+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«اللهُمَّ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ، فَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنَ المُسْلِمِينَ سَبَبْتُهُ أَوْ لَعَنْتُهُ أَوْ جَلَدْتُهُ فَاجْعَلْهَا لَهُ زَكَاةً وَرَحْمَةً».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2601]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Ewe Mola wangu, hakika mimi ni mwanadamu, basi yeyote katika Waislamu niliyemtukana au kumlaani au kumpiga kwa mjeledi, basi hilo lifanye kwake kuwa ni utakaso na huruma".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2601]

Ufafanuzi

Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Mola wangu, hakika mimi ni mwanadamu, hivyo basi, muumini yeyote niliyemuudhi au kumtukana au kumshutumu, au kumlaani, na nikamuombea kufukuzwa katika rehema yako, au nilimpiga mjeledi au kipigo chochote, basi lifanye hilo kwake kuwa ni utakaso na ibada na twahara na kafara na rehema utakayomhurumia kwayo.

Katika Faida za Hadithi

  1. Utukufu wa tabia ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Amesema bin Hajari: Katika hadithi kuna ukamilifu wa huruma yake rehema na amani ziwe juu yake juu ya Umma wake na uzuri wa tabia yake na ukarimu wake, kiasi kwamba alikusudia kuyakabili yaliyotokea kwake kama ponyo na ukarimu.
  3. Amesema Nawawi: Pakisemwa: Kwa nini amuombee dua mbaya asiyestahiki, au amtukane au amlaani na mfano wa hayo? Jawabu ni lile walilojibu wanachuoni, na kwa ufupi, liko namna mbili: Ya kwanza: Ni kuwa makusudio yake si wastahiki wa hilo mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hata undani wa jambo, lakini kwa uwazi wa jambo ni kuwa anastahiki hilo, inamdhihirikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa anastahiki hilo kwa alama za kisheria, kumbe uhalisia wake ni kinyume na hivyo, naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrishwa kuhumu kwa kile kinachodhihiri, na Mwenyezi Mungu ndiye anayesimamia siri. Ya pili: Ni kwamba kilichotokea katika kutusi kwake na dua yake mbaya na mfano wake, si makusudi, bali ni katika yale ambayo ndimi za Waarabu zilizoea katika kuunga kwao maneno yao pasina kukusudia, kama mtu kusema: Umepata hasara, au ushindwe kabisa, na katika hadithi hii: "Usiendelee kukua umri wako" na katika hadithi ya Muawia: "Mwenyezi Mungu asilishibishe tumbo lako" na mfano wa hayo hawakusudii chochote katika dua mbaya, akahofia Mtume rehema na amani ziwe juu yake maneno hayo yasijekukutana na muda wa kujibiwa dua yakampata mtu, akamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akajipendekeza kwake ili ayafanye hayo yote kuwa rehema na kafara, na ibada na twahara na malipo, bali yalikuwa yakijitokeza haya kwake kwa nadra sana na nyakati ndogo, na hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye ulimi mchafu wala mtoa laana, wala mwenye kulipiza kisasi kwa masilahi ya nafsi yake.
Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kikurdi Kireno Thai Kiassam الهولندية الدرية المجرية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama