عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ:
أَنَّ نَبِيَّ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ إِلَى كِسْرَى، وَإِلَى قَيْصَرَ، وَإِلَى النَّجَاشِيِّ، وَإِلَى كُلِّ جَبَّارٍ يَدْعُوهُمْ إِلَى اللهِ تَعَالَى، وَلَيْسَ بِالنَّجَاشِيِّ الَّذِي صَلَّى عَلَيْهِ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ.
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1774]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-:
Ya kwamba Nabii wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake aliandika ujumbe kwenda kwa Kisra, na Kaisari na kwenda kwa Najashi, na kwa kila jabari, akiwaita wote kuja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na si kwa Najashi yule aliyemswalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1774]
Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake, ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliandika ujumbe kabla ya kifo chake kwa Wafalme wa mataifa waliopembezoni mwake, akiwaita katika Uislamu; akamuandikia Kisra, nalo ni jina la kupachikwa la kila Mfalme Uajemi, na kwenda kwa Kaisari, nalo ni jina la kupachikwa kwa kila mfalme wa Roma, na kwenda kwa Najashi nalo ni jina la kupachikwa la kila mfalme wa uhabeshi. Na akaandika pia kwenda kwa kila mfalme jeuri mwenye kuwakandamiza watu, na mwenye kuwatenza nguvu, na akabainisha Anasi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Najashi aliyetumiwa Ujumbe si Najashi yule aliyesilimu na akafariki na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamswali swala ya maiti asiyekuwepo.