عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ:
لَمَّا نَزَلَتْ: {إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا لِيَغْفِرَ لَكَ اللهُ} إِلَى قَوْلِهِ {فَوْزًا عَظِيمًا} [الفتح: ١-٥] مَرْجِعَهُ مِنَ الْحُدَيْبِيَةِ، وَهُمْ يُخَالِطُهُمُ الْحُزْنُ وَالْكَآبَةُ، وَقَدْ نَحَرَ الْهَدْيَ بِالْحُدَيْبِيَةِ، فَقَالَ: «لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَيَّ آيَةٌ هِيَ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنَ الدُّنْيَا جَمِيعًا».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1786]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Ilipoteremka: "Hakika Sisi tumekufungulia wewe, ewe Mtume, ufunguzi ulio waziwazi, ili akusamehe Mwenyezi Mungu" mpaka katika kauli yake: "Ushindi mkubwa" [Fat-hi: 1-5] marejeo ya hili ni katika suluhu ya Hudaibia, na wao wakiwa wamejawa na huzuni na unyonge, na alichinja vichinjwa vyake hapo Hudaibia, akasema: "Hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya ninayoipenda zaidi kuliko dunia nzima".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1786]
Ameeleza Anasi bin Maaliki radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba ilipoteremka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kauli yake Mtukufu: "Hakika sisi tumekufungulia ewe Muhammadi ufunguzi wa wazi wazi (1) Ili akusameheme Mwenyezi Mungu yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika njia iliyonyooka (2) Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu (3) Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi imani juu ya imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye ujuzi, mwenye hekima (4) Ili awaingize Waumini wanaume na Waumini wanawake katika Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo, na awafutie makosa yao. Na huko ndiko kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (5) [Al-Fat-hi: 1-5]. Hili lilikuwa Wakati wa kurejea kwake kutoka Hudaibia, na wakati Maswahaba wakiwa wamegubikwa na huzuni na unyonge, wakiwa wamezuiliwa kutekeleza Umra, kwa sababu ya yale waliyokubaliana katika mkataba, na dhana yao ilikuwa; yote hayo hayana masilahi na Waislamu, na walichinja vichinjwa vyao hapo Hudaibia, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwa hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya inayopendeka zaidi kwangu kuliko dunia nzima, kisha akaisoma.