عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ:
كُنَّا فِي غَزَاةٍ فَكَسَعَ رَجُلٌ مِنَ المُهَاجِرِينَ رَجُلًا مِنَ الأَنْصَارِ، فَقَالَ الأَنْصَارِيُّ: يَا لَلْأَنْصَارِ، وَقَالَ المُهَاجِرِيُّ: يَا لَلْمُهَاجِرِينَ، فَسَمَّعَهَا اللَّهُ رَسُولَهُ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا هَذَا؟» فَقَالُوا: كَسَعَ رَجُلٌ مِنَ المُهَاجِرِينَ رَجُلًا مِنَ الأَنْصَارِ، فَقَالَ الأَنْصَارِيُّ: يَا لَلْأَنْصَارِ، وَقَالَ المُهَاجِرِيُّ: يَا لَلْمُهَاجِرِينَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «دَعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ» قَالَ جَابِرٌ: وَكَانَتِ الأَنْصَارُ حِينَ قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَكْثَرَ، ثُمَّ كَثُرَ المُهَاجِرُونَ بَعْدُ، فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَيٍّ: أَوَقَدْ فَعَلُوا، وَاللَّهِ لَئِنْ رَجَعْنَا إِلَى المَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ الأَعَزُّ مِنْهَا الأَذَلَّ، فَقَالَ عُمَرُ بْنُ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: دَعْنِي يَا رَسُولَ اللَّهِ أَضْرِبُ عُنُقَ هَذَا المُنَافِقِ، قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «دَعْهُ، لاَ يَتَحَدَّثُ النَّاسُ أَنَّ مُحَمَّدًا يَقْتُلُ أَصْحَابَهُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4907]
المزيــد ...
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao (yeye na baba yake), amesema:
Tulikuwa vitani, mtu mmoja katika Muhajirina akampiga mmoja katika Answari, Answari akasema: Maanswari naombeni msaada!, na akasema Mhajiri (mtu wa Makka): Naombeni msaada enyi Muhajirina!, Mwenyezi Mungu akamsikilizisha sauti zile Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Nini hiki?" Wakasema: Mtu mmoja miongoni mwa Muhajirina kampiga mtu katika Maanswari, akasema Answari: Naombeni msaada enyi Maanswari, na akasema Mhajiri: Naombeni msaada enyi Muhajirina, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Achaneni (na ubaguzi) kwani una nuka" Amesema Jabiri: Na Maanswari walikuwa wengi kipindi alipofika Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha Muhajirina wakawa wengi baada ya hapo, akasema Abdallah bin Ubaiyi: Vipi wamepigana? Na Wallahi tukirejea Madina watukufu watawafurusha madhalili, akasema Omari bin Khattwabi: Naomba uniache mimi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nikate shingo ya huyu mnafiki, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Muache ili watu wasiseme Muhammadi anauwa Maswahaba zake".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4907]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa safarini katika vita na akiwa pamoja na Maswahaba zake miongoni mwa Muhajirina na Maanswari radhi za Allah ziwe juu yao, mtu mmoja katika Muhajirina akampiga mgongoni mtu mmoja miongoni mwa Maanswari kwa mkono wake. Answari akasema: Nipeni msaada enyi Maanswari, na akasema Muhajiri: Nipeni msaada enyi Muhajirina, akawasikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Nini hiki?. Wakasema: Mtu mmoja katika Muhajirina kampiga mtu katika Maanswari kwa mkono wake, Answari akasema: Nipeni msaada enyi Maanswari, na Muhajiri akasema: Nipeni msaada enyi Muhajirina. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Achaneni na desturi hii ya kijinga, kwani ni mbaya inachukiza na ina udhi; nayo ni kwamba mtu akizidiwa na mgomvi wake anawaita watu wake wanaanza kumsaidia sawa sawa awe kadhulumu au kadhulumiwa, kwa sababu ya ujinga wao, na ubaguzi wao. Amesema Jabiri: Na Maanswari wakati amefika Mtume rehema na amani ziwe juu yake mji wa Madina walikuwa wengi, kisha Muhajirina wakawa wengi baada ya hapo. Akasema kiongozi wa unafiki Abdallah bin Ubai bin Saluli: Jambo limefikia huko?! Wallah tukirejea Madina watukufu (anajikusudia yeye na watu wake) watawatoa katika mji wa Madina madhalili (anakusudia Mtume rehema na amani ziwe juu yake na watu wake). Akasema Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake: Hebu, niache ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nikate shingo ya huyu mnafiki, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Muache, ili watu wasiseme kuwa Muhammadi anauwa wafuasi wake, hata kama ni kwa dhahiri.