+ -

عن أبي سفيان صخر بن حرب رضي الله عنه قال: قال هِرَقل: فماذا يَأمُرُكُم -يعني: النبي صلى الله عليه وسلم- قال أبو سفيان: قلت: يقول: «اعبدُوا الله وَحدَه لاَ تُشرِكُوا بِهِ شَيئًا، وَاترُكُوا ما يَقُول آبَاؤُكُم، ويَأمُرُنَا بِالصَّلاَة، والصِّدق، والعَفَاف، والصِّلَة».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Sufiyan Swakhar bin Harbi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: alisema Hiraqli: Hivi anawaamrisha nini? Yaani: Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake, akasema Abuu Sufiyani nikasema: "Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake msimshirikishe yeye na chochote, na acheni wanayosema baba zenu, na anatuamrisha swala na ukweli, na kujizuia na machafu, na kuunga udugu".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

Ufafanuzi

Haya ni mazungumzo ya Abuu sufiyani Swakhar bin Harbi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- ambayo ni mashuhuri yeye pamoja na Hiraqli, alikuwa Abuu Sufiyani wakati huo ni mshirikina, kiasi kwamba hakusilimu ila kwa kuchelewa, ilikuwa ni kati ya sulhul Hudaibiya (mkataba wa makubaliano wa Hudaibiya) na Fat-hu Makka (kufunguliwa kwa mji wa Makka) alitoka Abuu Sufiyani akiwa pamoja na kundi la makuraishi wakielekea kwa Hiraqli katika mji wa Sham, na Hiraqli alikuwa ni mfalme wa wakristo kwa wakati ule, na alikuwa amesoma katika taurati na Injili na vitabu vilivyotangulia, na alikuwa ni mfalme mwerevu, basi aliposikia ujio wa Abuu Sufiyani na wale walio pamoja naye, nao wakitokea katika miji ya jangwani aliwaita, na akaanza kuwauliza kuhusu hali ya Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- na kuhusu nasaba (ukoo) wake, na kuhusu maswahaba zake, na jinsi gani wanavyomuheshimu, na uaminifu wake Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- basi wanapotaja kitu wanachomueleza anazidi kujua kuwa huyu ndiye Nabii aliyeelezwa katika vitabu vilivyotangulia, lakini yeye -Tunamuomba Allah atuepushe na hilo- ni mtu mwenye uchu na ufalme wake akawa hakusilimu kwa hekima alizozitaka Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ilikuwa miongoni mwa yale aliyomuuliza Abuu Sufiyani ni kumuuliza juu ya yale anayoyaamrisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamueleza kuwa yeye anawaamrisha wao wamuabudu Mwenyezi Mungu na wala wasimshirikishe yeye na chochote, basi wasiabudu zaidi ya Mwenyezi Mungu, si Malaika wala Mtume, na wala si mti wala jiwe, na wala si jua wala mwezi, na wala si kinginecho, ibada zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, na huu ndio ujumbe wa Mtume, akaja Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na yale waliyokuja nayo Mitume kabla yake, kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika. Na akisema: "Yaacheni waliyokuwa nayo baba zenu" na hii ni katika kuutangaza ukweli, yale yote yaliyokuwa kwa baba zao katika kuabudu masanamu, aliwaamrisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuyaacha, na ama yale waliyokuwa nayo baba zao katika tabia njema; basi hakuwaamrisha wayaache. Na kauli yake: "Na alikuwa akituamrisha kuswali" swala ni mawasiliano kati ya mja na Mola wake, nayo ni nguzo ya pili yenye mkazo baada ya shahada mbili, na kupitia hii anajulikana muumini na kafiri, hiyo ndiyo ahadi iliyoko kati yetu na washirikina na makafiri, kama alivyosema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Ahadi iliyoko kati yetu sisi na wao ni swala, atakayeiacha atakuwa kakufuru" Na kauli yake: "Na alikua akituamrisha ukweli" Yaani alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiuamrisha umma wake kuwa wakweli, na hii ni kama kauli yake Mtukufu: "Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na muwe miongoni mwa wakweli", na ukweli ni tabia njema, na unagawanyika sehemu mbili: kuwa mkweli pamoja na Mwenyezi Mungu, na kuwa mkweli pamoja na waja wa Mwenyezi Mungu, na yote mawili ni katika tabia njema. Na kauli yake "Na kujizuia na machafu" Yaani kujizuia na machafu kuna aina mbili: ni kujizuia na matamanio ya tupu, na kujizuia na matamanio ya tumbo. Na ama kujizuia kwa kwanza: nako ni mtu ajizuie na yale aliyoharamishiwa kama zinaa na njia zake na vishawishi vyake. Na ama aina ya pili ya kujizuia: nayo kujizuia kutokana na matamanio ya tumbo, yaani ni kujizuia na vile vilivyoko mikononi mwa watu, na kujizuia kutowaomba, kiasi kwamba mtu hamuombi yeyote chochote; kwasababu kuomba omba ni udhalili, na muombaji mkono wake uko chini, na mtoaji mkono wake uko juu, haifai kumuomba yeyote isipokuwa kwa yale ambayo hayana budi. Ama kauli yake: "kuunga udugu": nako ni mtu kuunga yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu ayaunge katika udugu wa karibu kisha unaofuata, na ndugu wa karibu zaidi ni wazazi wawili, kwani kuwaunga wazazi wawili ni wema na ni kuwaunga, na ndugu wa karibu wana haki ya kuungwa kulingana na ukaribu wao utakavyokuwa, kaka ana haki zaidi kuliko baba mdogo, na baba mdogo ana haki zaidi kuliko baba yake mdogo na baba, na kuunga udugu kunakuwa kulingana na jinsi watu walivyozoea.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama