عَنِ ‌ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما:
أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَطَبَ النَّاسَ يَوْمَ فَتْحِ مَكَّةَ، فَقَالَ: «يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّ اللهَ قَدْ أَذْهَبَ عَنْكُمْ عُبِّيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ وَتَعَاظُمَهَا بِآبَائِهَا، فَالنَّاسُ رَجُلَانِ: بَرٌّ تَقِيٌّ كَرِيمٌ عَلَى اللهِ، وَفَاجِرٌ شَقِيٌّ هَيِّنٌ عَلَى اللهِ، وَالنَّاسُ بَنُو آدَمَ، وَخَلَقَ اللهُ آدَمَ مِنْ تُرَابٍ، قَالَ اللهُ: {يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ} [الحجرات: 13]».

[صحيح] - [رواه الترمذي وابن حبان]
المزيــد ...

Na kutoka kwa Ibn Omari Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake:
Ya kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwahutubia watu siku ya ufunguzi wa mji wa Makka, akasema: "Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba , basi watu wako aina mbili: Mwema mchamungu mtukufu kwa Mwenyezi Mungu, na muovu mbaya dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na watu wote ni wana wa Adam, na amemuumba Mwenyezi Mungu Adam kutokana na udongo. Amesema Mwenyezi Mungu: "Enyi watu hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila tofauti tofauti, ili mfahamiane, hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana habari (za mambo yote)" [Al Hujuraat: 13].

Sahihi - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy

Ufafanuzi

Aliwahutubia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- watu siku ya ufunguzi wa mji wa Makka akasema: Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu amenyanyua na akaondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga na kujiona, na kujifaharisha kwa baba zenu (nasaba), bali watu wako aina mbili:
Ni ima muumini mwema, mchamungu, mtiifu, mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, huyu ni mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, hata kama hana cheo au nasaba nzuri mbele za watu.
Na ima kafiri muovu, na huyu ni dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na wala hana thamani yoyote, hata kama ana ukoo mzuri na cheo na mamlaka.
Na watu wote ni watoto wa Adam, na Mwenyezi Mungu kamuumba Adam kutokana na udongo, haifai kwa kiumbe ambaye asili yake ni udongo kuwa na kiburi na kujiona yeye ni bora, na hili linasadikishwa na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi watu! hakika sisi tumekuumbeni nyinyi kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila ili mpate kujuana, hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana habari (ya myafanyayo) [Alhujrat:13].

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Kibangali Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Katazo la kujifaharisha kwa ukoo na vyeo.