عَنْ الزُّبَيْرِ بْنِ الْعَوَّامِ قَالَ:
لَمَّا نَزَلَتْ: {ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ} [التكاثر: 8]، قَالَ الزُّبَيْرُ: يَا رَسُولَ اللهِ، وَأَيُّ النَّعِيمِ نُسْأَلُ عَنْهُ، وَإِنَّمَا هُمَا الْأَسْوَدَانِ التَّمْرُ وَالْمَاءُ؟ قَالَ: «أَمَا إِنَّهُ سَيَكُونُ».
[حسن] - [رواه الترمذي وابن ماجه] - [سنن الترمذي: 3356]
المزيــد ...
Kutoka kwa Zubairi bin Awwam amesema:
Ilipoteremka: "Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema" [Takathur: 8], akasema Zubairi: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni neema zipi tutakazooulizwa juu yake, au ni hivi vyeusi viwili tende na maji (Vyakula na vinywaji kwa ujumla)? Akasema: "Hakika bila shaka zitakuwa hizo".
[Ni nzuri] - - [سنن الترمذي - 3356]
Ilipoteremka aya: "Kisha hakika bila shaka mtaulizwa siku hiyo kuhusu neema" Yaani: Mtakuja kuulizwa kuhusu kutekeleza shukurani kwa yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu juu yenu miongoni mwa neema, akasema Zubairi bin Awwam radhi za Allah ziwe juu yake: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni neema zipi tutakazoulizwa juu yake?! Ni neema mbili ambazo hazihitaji kuziomba ambazo ni tende na maji!.
Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ama hakika nyinyi mtaulizwa kuhusu neema pamoja hali hii iliyo nayo, ni hizi neema mbili kubwa katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu.