Aina ndogo

Orodha ya Hadithi

Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamfutia deni, Allah atampa kivuli siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, hamtokingwa katika kumuona kwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hivi nisikuelezeni watu wa peponi? Kila mnyonge mwenye kujishusha, na lau kama angeliapia kwa Mwenyezi Mungu basi angelimuepusha (na kutopokea kiapo chake), hivi nisikuelezeni watu wa motoni? kila jeuri mkaidi mwenye kiburi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakika atakuja mtu mnene tena mkubwa siku ya kiyama akiwa halingani mbele ya Mwenyezi Mungu hata na uzito wa bawa la mbu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katika mambo yapi? Na kuhusu elimu yake aliifanyia kazi katika nini? Na kuhusu mali yake ni wapi aliichuma? Na aliitoa katika mambo gani? Na kuhusu mwili wake aliumaliza katika mambo yapi?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Je mnajua ni nani aliyefilisika?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakuna mwenye kumiliki dhahabu wala fedha, na akawa hazitolei zaka zake, isipokuwa, pindi itakapofika siku ya Kiyama, atakunjiwa Sahani la kutoka motoni
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za wema wake hapa Duniani na hulipwa thawabu hizo huko Akhera
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Kwa hakika mimi nitakuwa kwenye Birika langu namtazama kila mwenye kuja kwangu kunywa, na kuna watu watafukuzwa, na nitasema: Ewe Mola wangu huyu anatokana na mimi na ni katika umma wangu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Jua litasogezwa karibu na viumbe Siku ya Kiyama mpaka liwe karibu nao umbali wa maili moja
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Mwenyezi Mungu atawakusanya watu wa mwanzo na mwisho katika udongo mmoja, atawasikilizisha mwenye kunadi, na atawapa upeo wa kuona, na jua linaposogea, watu watafikwa na tabu na matatizo kiasi ambacho hawatoweza kuvumilia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakika kundi la kwanza la watu watakaoingia peponi watakuwa katika sura ya mwezi usiku wa tarehe kumi na tano, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali ing'aayo na iangazayo mbinguni
عربي Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala
Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi
عربي Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala