+ -

عَنِ الْمِقْدَادِ بْنِ الْأَسْوَدِ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ:
«تُدْنَى الشَّمْسُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنَ الْخَلْقِ، حَتَّى تَكُونَ مِنْهُمْ كَمِقْدَارِ مِيلٍ»، قَالَ سُلَيْمُ بْنُ عَامِرٍ: فَوَاللهِ مَا أَدْرِي مَا يَعْنِي بِالْمِيلِ؟ أَمَسَافَةَ الْأَرْضِ، أَمِ الْمِيلَ الَّذِي تُكْتَحَلُ بِهِ الْعَيْنُ قَالَ: «فَيَكُونُ النَّاسُ عَلَى قَدْرِ أَعْمَالِهِمْ فِي الْعَرَقِ، فَمِنْهُمْ مَنْ يَكُونُ إِلَى كَعْبَيْهِ، وَمِنْهُمْ مَنْ يَكُونُ إِلَى رُكْبَتَيْهِ، وَمِنْهُمْ مَنْ يَكُونُ إِلَى حَقْوَيْهِ، وَمِنْهُمْ مَنْ يُلْجِمُهُ الْعَرَقُ إِلْجَامًا» قَالَ: وَأَشَارَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِيَدِهِ إِلَى فِيهِ.

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2864]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Mikidadi bin Aswadi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Jua litasogezwa karibu na viumbe Siku ya Kiyama mpaka liwe karibu nao umbali wa maili moja.", Sulaim bin 'Amir akasema: "Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, sijui (kiwango) alimaanisha nini kwa "maili"? Je, ni umbali katika ardhi au ni kile kijiti kinachotumiwa kupaka wanja wa manga kwenye jicho." (Mtume) Akasema: "Kisha, watu watakuwa ndani ya jasho yao kulingana na matendo yao. Miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye vifundo viwili vya miguu yake. Na miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye magoti yake mawili. Na miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye nyonga zake mbili. Na miongoni mwao, kuna ambaye jasho (lake) litammeza kabisa."

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2864]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Jua litasogezwa siku ya Kiyama karibu na viumbe, mpaka liwe vichwani mwao kwa kiasi cha maili moja. Amesema taabii (Mwanafunzi wa swahaba) Saidi bin Aamiri: Wallahi sijui ni maili mbili zipi alikusudia, je ni masafa ya ardhi, ama ni maili (wanja) ambao hutumika kupaka macho? Akasema: Watakuwa katika jasho kulingana na amali zao; yuko miongoni mwao ambaye jasho lake litatiririka mpaka chini ya kongo mbili zake za miguu, na yuko ambaye jasho lake litatiririka mpaka magotini, na yuko ambaye jasho litakuwa katika kitovu chake na kiunoni kwake, na yuko ambaye jasho litafika katika mdomo wake na litamzuia kuzungumza. Amesema: Na akaashiria rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake katika kinywa chake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Thai Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa misukosuko ya siku ya Kiyama na kuogopeshwa nayo.
  2. Watu watakuwa katika shida siku ya Kiyama katika kisimamo kulingana na hesabu ya matendo yao.
  3. Himizo la kufanya matendo ya kheri, kemeo la kutofanya matendo ya shari.