عن جرير بن عبد الله البجلي رضي الله عنه قال: كنا عندَ النبيِّ صلى الله عليه وسلم فنظرَ إلى القمرِ ليلةَ البدرِ، فقالَ: «إنَّكم سترون ربَّكُمْ كما تروْن هذا القمر، لاَ تُضَامُونَ في رُؤْيَته، فَإن استطعتم أنْ لاَ تُغْلَبُوا على صلاة قبل طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا، فَافْعَلُوا». وفي رواية: «فنظر إلى القمر ليلة أربع عشرة».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Jariri bin Abdillah Al-bajaliy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Tulikuwa kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- akautazama mwezi usiku wa tarehe kumi na nne (14), Akasema: "Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, Hamtopata tabu katika kumuona kwake, basi ikiwa mtaweza kutozidiwa na kuswali kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama kwake basi fanyeni hivyo" na katika riwaya: "Akautazama mwezi usiku wa tarehe kumi na nne".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Kutoka kwa Jariri bin Abdillah Al-bajaliy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba wao walikuwa pamoja na Mtume Rehema na Amani ziwe kwake- Akautazama mwezi usiku wa kati kati ya mwezi- yaani usiku wa tarehe kumi na nne- Akasema Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona huu mwezi" Yaani: siku ya kiyama na peponi watamuona wachamungu kama wanavyouona mwezi usiku wa kati kati ya mwezi, haina maana kuwa Mwenyezi Mungu ni kama mwezi; kwasababu Mwenyezi Mungu hakuna kitu chochote mfano wake, bali yeye ni mkubwa na Mtukufu aliyetukuka, Lakini makusudio ya kuona hapa ni kufananisha (namna ya) kuona kwa kuona, si kinachoonekana kwa kinachoonekana, kama jinsi tunavyouona mwezi wa tarehe za kati kati kuuona ambako ni kwa uhakika hakuna usumbufu ndani yake, basi hakika sisi tutamuona Mola wetu -Aliyetakasika na kutukuka- kama jinsi tunavyouona mwezi kuuona kiuhalisia kwa macho bila usumbufu, na neema tamu na neema nzuri kwa watu wa peponi kuuangalia uso wa Mwenyezi Mungu hakuna kitu kinacholingana na hilo, basi anasema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kwa kile alichokitaja kuwa sisi tutamuona Mola wetu kama tunavyouona mwezi wa tarehe za kati kati: "basi ikiwa mtaweza kutozidiwa na kuswali kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama kwake basi fanyeni hivyo", Na makusudio ya kauli yake: "basi ikiwa mtaweza kutozidiwa na kuswali": Yaani: katika kuzitekeleza swala hizo mbili zikiwa kamili, na miongoni mwake: ni kuziswali katika jamaa, mkiweza kutozidiwa juu ya hili, "Basi fanyeni", na katika hili kuna dalili kuwa kuhifadhi swala ya Al-fajiri na swala ya Laasiri ni katika sababu za kuutazama uso wa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.