عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «مَنْ أَنْظَرَ مُعْسِرا، أو وضع له، أظَلَّهُ الله يوم القيامة تحت ظِل عرشه يوم لا ظِلَّ إلا ظِلُّه».
[صحيح] - [رواه الترمذي والدارمي وأحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamsamehe, atampa kivuli Mwenyezi Mungu siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hakutokuwa na kivuli ispokuwa kivuli chake".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy
Ameeleza Abuu Huraira kuwa Mtume rehema na Amani ziwe juu yake Amesema: "Atakayempa muda mwenye hali ngumu" Yaani akampa nafasi mdaiwa masikini, kutoa muda ni kuchelewesha kunakotazamiwa kusamehe. Kauli yake "Au akamsamehe" Yaani akamfutia katika deni lake, na katika riwaya ya Abuu Nuaim "Au akampa zawadi". Hivyo malipo ni: "Atampa kivuli Mwenyezi Mungu siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake" Yaani atampa kivuli katika kivuli cha Arshi yake halisia au atamuingiza peponi; Atamkinga Mwenyezi Mungu na joto la siku ya kiyama. Na malipo haya yatakuwa: "Siku ambayo kutokuwa na kivuli ispokuwa kivuli chake" Yaani kivuli cha Mwenyezi Mungu, na hakika amestahiki mtoa muda jambo hilo kwasababu ya kumpendelea mdaiwa kuliko nafsi yake na akampumzisha na Mwenyezi Mungu akampumzisha, na malipo huendana na matendo.