عن أبي هريرة - رضي الله عنه- مرفوعاً: «من أنْفَق زوْجَيْن في سَبيل الله نُودِي من أبْوَاب الجنَّة، يا عبد الله هذا خَيْرٌ، فمن كان من أهل الصلاة دُعِي من باب الصلاة، ومن كان من أهل الجِهاد دُعِي من باب الجِهاد، ومن كان من أهل الصيام دُعِي من باب الرَّيَّانِ، ومن كان من أهل الصَّدَقة دُعِي من باب الصَّدَقة» قال أبو بكر رضي الله عنه : بأبي أنت وأمي يا رسول الله! ما على من دُعِي من تلك الأبواب من ضَرورة، فهل يُدْعَى أحَدٌ من تلك الأبواب كلِّها؟ فقال: «نعم، وأرْجُو أن تكون منهم».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- hadithi Marfu'u: "Atakayetoa jinsia (aina) mbili katika njia ya Mwenyezi Mungu huitwa katika milango ya pepo, ewe mja wa Mwenyezi Mungu hii ni kheri, hivyo atakayekuwa miongoni mwa watu wa swala ataitwa katika mlango wa swala, atakayekuwa katika watu wa jihadi ataitwa katika mlango wa jihadi, atakayekuwa miongoni mwa watu wa swaumu ataitwa katika mlango wa Rayyan, atakayekuwa miongoni mwa watu wa sadaka ataitwa katika mlango wa sadaka" Akasema Abuubakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Namuweka fidia baba yangu na mama yangu kwaajili yako, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! je kama kuna mtu ataitwa katika milango hiyo akawa na dharura, je anaweza kuitwa mtu katika milango hiyo yote? basi akasema: "Ndiyo, na ninataraji wewe utakuwa miongoni mwao".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Atakayetoa sadaka kwa vitu viwili katika vitu vyovyote, mfano kama vyakula au mavazi au kipando au pesa, kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu humuita Malaika katika milango ya pepo wakimkaribisha kuelekea katika milango hiyo, nao wakisema: Hakika umetanguliza kheri nyingi unalipwa kwazo leo malipo makubwa. Wale wenye kukithirisha swala wataitwa katika mlango wa swala, na wataingia hapo, na wenye kukithirisha sadaka wataitwa katika mlango wa sadaka, na wataingia hapo, na wenye kukithirisha kufunga Malaika watawapokea katika mlango wa Rayyan wakiwaita kuingia hapo, na maana ya Rayyan: ni mtu anayekata kiu; kwasababu wafungaji hujizuia na kunywa maji wakapatwa na kiu na hasa hasa katika siku za kiangazi kirefu na chenye joto, hivyo watalipwa kwa kiu yao kwa kukatwa kiu milele katika pepo ambayo wataingia kupitia mlango huo. Aliposikia Abuubakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwake- mazungumzo haya, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, "fidia yako namtoa baba yangu na mama yangu" atakayeingia katika milango hii hatokuwa na mapungufu wala hasara, kisha akasema: "Je inawezekana mtu akaitwa katika milango hiyo yote?" Akasema -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ndiyo, na ninataraji wewe kuwa miongoni mwao".

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama