عن سهل بن سعد رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«مَنْ يَضْمَنْ لِي مَا بَيْنَ لَحْيَيْهِ وَمَا بَيْنَ رِجْلَيْهِ أَضْمَنْ لَهُ الْجَنَّةَ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6474]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Sahal Ibn Sa'd -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Yeyote atakayenidhaminia mimi vilivyo kati ya Taya mbili na vilivyo kati ya miguu yake ninampa dhamana ya Pepo".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6474]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili nayo muislamu basi ataingia Peponi,
La kwanza: Kuhifadhi ulimi kutozungumza yale yenye kumchukiza Allah Mtukufu,
La pili: Kuhifadhi tupu kutotumbukia katika machafu;
Kwa sababu viungo viwili hivi hukithiri kutokea maasi kwavyo.