عن عَائِشَةَ رضي الله عنها قالت: ((كُنْتُ أَغْتَسِلُ أَنَا ورسول الله صلى الله عليه وسلم مِن إِنَاءٍ وَاحِدٍ، كِلاَنَا جُنُب، وكان يَأْمُرُنِي فَأَتَّزِرُ، فَيُبَاشِرُنِي وأنا حَائِض، وكان يُخْرِج رَأسَه إِلَيَّ، وهُو مُعْتَكِفٌ، فَأَغْسِلُهُ وأنا حَائِض)).
[صحيح] - [متفق عليه، لكنه روي مفرقًا، فمن أول الحديث إلى قولها"كلانا جنب": رواه البخاري، ومسلم. من قولها"وكان يأمرني" إلى قولها:"وأنا حائض": متفق عليه، رواه: البخاري، ومسلم. آخر الحديث: متفق عليه، رواه: البخاري، ومسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba, na alikuwa akiniamrisha najifunga kikoi(kishida), ananigusa na mimi nikiwa katika hedhi, na alikuwa akitoa kichwa chake kwangu, naye akiwa katika itikafu (msikitini), ninamuosha nami nikiwa katika hedhi".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yeye na mkewe Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- wakioga kutokana na janaba katika chombo kimoja, kwasababu maji ni twahara (ni masafi) hayadhuriwi na mchoto wa mwenye janaba, atakapokuwa kaiosha mikono yake kabla ya kuiingiza katika chombo. Na alitaka Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuweka sheria kwa umma wake kuwa karibu na mwanamke mwenye hedhi baada yakuwa mayahudi walikuwa hawali naye, na wala hawalali naye, basi akawa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akimuamrisha Aisha anajifunga kikoi, anamgusa mwili wake bila kufanya tendo la ndoa, hali yakuwa naye akiwa katika hedhi. Na alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akikaa itikafu anakitoa kichwa chake kwa Aisha naye akiwa msikitini anakiosha, ukaribu na mwenye hedhi hakuna tatizo katika mfano wa mambo kama haya, na alileta sheria hii kama kuwapa fursa watu baada yakuwa mahayudi wamewabana, lakini mwenye hedhi haingii msikitini, ili asipachafue, kama ilivyokuja katika hadithi hii.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama