عَنْ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
نَظَرْتُ إِلَى أَقْدَامِ الْمُشْرِكِينَ عَلَى رُءُوسِنَا وَنَحْنُ فِي الْغَارِ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ لَوْ أَنَّ أَحَدَهُمْ نَظَرَ إِلَى قَدَمَيْهِ أَبْصَرَنَا تَحْتَ قَدَمَيْهِ، فَقَالَ: «يَا أَبَا بَكْرٍ، مَا ظَنُّكَ بِاثْنَيْنِ اللهُ ثَالِثُهُمَا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2381]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abubakari Swiddiq radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Niliitazama miguu ya washirikina juu ya vichwa vyetu, na sisi tukiwa pangoni, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau kama mmoja wao angelitazama katika nyayo zake angetuona chini ya nyayo zake, akasema: "Ewe Abubakari, kwani ipi dhana yako kwa wawili ambao Mwenyezi Mungu ndiye wa tatu wao".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2381]
Alisema kiongozi wa waumini Abubakari Swiddiq radhi za Allah ziwe juu yake wakati wa kuhama: Nilitazama katika nyayo za washirikina nao wakiwa wamesimama juu ya vichwa vyetu juu ya pango na sisi tukiwa ndani yake, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau kama mmoja wao angelitazama katika nyayo zake angetuona chini ya nyayo zake, akasema: Ewe Abubakari, kwani ni ipi dhana yako kwa wawili ambao Mwenyezi Mungu ndiye wa tatu wao kwa kuwanusuru na kuwasaidia, na kuwahifadhi na kuwapa muongozo?!