+ -

عَنْ مُعَاذَةَ قَالَتْ:
سَأَلْتُ عَائِشَةَ، فَقُلْتُ: مَا بَالُ الْحَائِضِ تَقْضِي الصَّوْمَ، وَلَا تَقْضِي الصَّلَاةَ؟ فَقَالَتْ: أَحَرُورِيَّةٌ أَنْتِ؟ قُلْتُ: لَسْتُ بِحَرُورِيَّةٍ، وَلَكِنِّي أَسْأَلُ. قَالَتْ: كَانَ يُصِيبُنَا ذَلِكَ، فَنُؤْمَرُ بِقَضَاءِ الصَّوْمِ، وَلَا نُؤْمَرُ بِقَضَاءِ الصَّلَاةِ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 335]
المزيــد ...

Kutoka kwa Muadha amesema:
Nilimuuliza Aisha nikasema: Vipi kuhusu mwenye hedhi analipa swala na wala halipi swala? Akasema: Hivi wewe ni mtu kutoka Haruuraa? (mji walikozusha fitina baina ya waislamu) Akasema: Hapana: Mimi si mtu kutoka Haruuraa, bali mimi ninauliza tu, akasema: Tulikuwa tukipatwa na hilo, tunaamrishwa kulipa swaumu, na wala hatuamrishwi kulipa swala.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 335]

Ufafanuzi

Muadhi alimuuliza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Kwa nini mwenye hedhi analipa swaumu na wala halipi swala?. Akasema kumwambia: Hivi wewe ni katika Makhawariji (wanaotoka katika utiifu wa kiongozi wao) wa mji wa Haruuraa wanaokithirisha maswali kwa kutaka ugumu na kutia mkazo katika dini? Akasema: Mimi si mtu kutoka Haruuraa, bali mimi ninauliza tu, akasema: Tulikuwa tukipatwa na hedhi tukiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi tunaamrishwa kulipa swaumu, na wala hatuamrishiwi kulipa swala.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumkemea kila mwenye kuuliza swali la ukorofi na mjadala usio na faida.
  2. Haruuria imenasibishwa na mji ulioko karibu na Kufa (Iraq), na unaitwa "Haruuraa": kulikuwa na kundi la Makhawariji (wanaojitoa katika kumtii kiongozi wao), alimfananisha nao katika mambo yao, na wingi wa maswali yao, na ukaidi wao.
  3. Mwalimu anatakiwa kumbaini aliyemtaka kujifunza na kumpa muongozo.
  4. Kujibu kwa nukuu ni bora; kwa sababu Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu ziwe juu yake, hakujali maana aliyoikusudia muulizaji; na hii ni kwa sababu kujibu kwa hoja hukata zaidi mzozo.
  5. Kujisalimisha katika hukumu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, hata kama mja hatojua hekima yake.
  6. Amesema Nawawi: Maana ya kauli ya Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuwa kundi katika Makhawariji (wanaotoka katika kuwatii viongozi) humuwajibishia mwenye hedhi kulipa swala zilizompita wakati wa hedhi, jambo ambalo ni kinyume na makubaliano ya waislamu, na kiulizo hiki alichotumia Aisha kumuuliza ni kiulizo cha kumkemea mtu, yaani: Huu ni mfumo wa Haruria na ni mfumo mbaya mno.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama