عن أُمِّ عَطِيَّةَ رَضي الله عنها، وكَانَتْ بايَعَت النبيَّ صلى الله عليه وسلم، قالت:
كُنَّا لا نَعُدّ الكُدرَةَ والصُّفْرَةَ بعدَ الطُّهرِ شيئًا.
[صحيح] - [رواه أبو داود بهذا اللفظ، ورواه البخاري بدون زيادة (بعد الطهر)] - [سنن أبي داود: 307]
المزيــد ...
Kutoka kwa mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa kampa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema:
"Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote".
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 307]
Ameeleza swahaba mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake kuwa wanawake katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake walikuwa hawayazingatii maji maji yanayotoka katika tupu -ambayo yanaelekea katika weusi, au katika njano- baada ya kuona twahara ya kutoka katika hedhi: kuwa ni hedhi, hawaachi swala na swaumu kwa sababu yake.