عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤمنين رضي الله عنها أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ أَبِي حُبَيْشٍ سَأَلَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَتْ:
إِنِّي أُسْتَحَاضُ فَلاَ أَطْهُرُ، أَفَأَدَعُ الصَّلاَةَ؟ فَقَالَ: «لَا، إِنَّ ذَلِكِ عِرْقٌ، وَلَكِنْ دَعِي الصَّلاَةَ قَدْرَ الأَيَّامِ الَّتِي كُنْتِ تَحِيضِينَ فِيهَا، ثُمَّ اغْتَسِلِي وَصَلِّي».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 325]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Fatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema:
Mimi hupatwa na hedhi ya ugonjwa na sitwahariki, je niache swala? Akasema: "Hapana, hakika hilonitatizolinatokananamshipawakizazikukatika, lakini acha swala kwa kiasi cha siku ulizokuwa ukipata hedhi ndani yake, kisha oga na swali".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 325]
Fatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika mimi damu haikatiki kwangu na huendelea hata nje ya wakati wa hedhi, je itakuwa hukumu ya damu hiyo ni hukumu ya damu ya hedhi ili niache swala? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema kumwambia: Hiyo ni damu ya ugonjwa, nayo ni damu ya ugonjwa ambayo husababishwa na kukatika kwa mshipa katika mfuko wa uzazi, na si damu ya hedhi, Unapokuja muda wa hedhi uliokuwa ukipata hedhi ndani yake kwa mujibu wa ada yako ya mwezi kabla hujaugua, basi acha swala na swaumu na mengineyo anayozuiliwa kuyafanya mwenye hedhi wakati wa hedhi. Kinapomalizika kiwango cha muda huo, hapo utakuwa umetwaharika na hedhi, osha mahali palipo na damu, kisha osha mwili wako josho kamili kwa ajili ya kuondoa hadathi, kisha swali.