عَنْ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ:
أَنَّهُ جَاءَ إِلَى الحَجَرِ الأَسْوَدِ فَقَبَّلَهُ، فَقَالَ: إِنِّي أَعْلَمُ أَنَّكَ حَجَرٌ، لاَ تَضُرُّ وَلاَ تَنْفَعُ، وَلَوْلاَ أَنِّي رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُقَبِّلُكَ مَا قَبَّلْتُكَ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1597]
المزيــد ...
Kutoka kwa Omari -radhi za Allah ziwe juu yake-:
Ya kwamba siku moja alikuja katika jiwe jeusi akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama nisingemuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1597]
Alikuja kiongozi wa waumini Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake katika jiwe jeusi katika kona ya Kaaba akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama mimi nisingelimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.